IQNA

Waziri Mkuu wa Malaysia
14:32 - November 30, 2019
News ID: 3472243
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Malaysia Dakta Mahathir Mohammad amesema Waislamu wanapaswa kuwa na tabia njema na maadili bora ili kuwavutia wasiokuwa Waislamu katika Uislamu.

Ametoa wito kwa Waislamu kujiepusha na misimamo mikali, kutusi wafuasi wa dini au kaumu zigine na kuzozoana kwa ajili ya kutafautiana kimitazamo ili waweze kuuhubiri Uislamu.

"Wasiokuwa Waislamu hawatatukubali iwapo tutakuwa na sifa hasi na hatufanikiwi katika maisha. Tunapaswa kuoneysha sifa njema, na Inshallah, watavutiwa na vitendo vyetu na hivyo wauamini Uislamu," amesema Mahathir Mohammad.

Waziri Mkuu wa Malaysia amekosoa tabia ya baadhi ya Waislamu kuchochea uhasama na mifarakano na kusema muenendo huo si tu kuwa unaidhuru jamii bali huangamiza pia taifa.

Amesema iwapo mataifa ya Waislamu yatafeli basi kutaenezwa fikra kuwa Uislamu nao umefeli.

Akiashiria hali ya mambo katika eneo la Asia ya Kati (Mashariki ya Kati), Mahathir Mohammad amesema nchi za eneo hilo zinahasimiana pamoja na kuwa mataifa ya eneo hilo yanafuata dini moja.  Amesema wakati nchi za Waislamu zinapohasimiana maadui hutumia frusa hiyo na kuuzia pande hasimu silaha na hivyo kuibua vita na machafuko.

3860431

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: