IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tunisia

11:23 - December 14, 2019
Habari ID: 3472276
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Awamu ya 17 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tunisia wametangazwa katika sherehe iliyofanyika Ijumaa.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zimefanyika katika Msikiti wa Al Zaytuna katika mji mkuu, Tunis huku maafisa kadhaa wa ngazi za juu wakishiriki akiwemo waziri wa masuala ya kidini na Mufti Mkuu wa Tunisia pamoja na wanadiplomasia kutoka nchi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na jopo la majaji, qarii kutoka Algeria alishika nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa huku nafasi ya pili ikishikiwa na Hussein Poorkavir wa Iran naye mwakilishi wa Uturuki alishika nafasi ya tatu.

Mashindano hayo yalianza mjini Tunis Jumamosi iliyopita ambapo kulikuwa na wawakilishi 21. Mashindano yam waka huu yamepewa jina la Imam Hassan bin Khalaf bin Balima Kairouani, ambaye ni Mtunisia aliyekuwa mashuhuri katika qiraa au usomaji Qur'ani Tukufu katika karne ya 11 Miladia.

3863746

captcha