IQNA

15:29 - December 26, 2019
News ID: 3472306
TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wawili nchini Thailand ambao waliwapiga risasi na kuwaua Waislamu watatu kusini mwa nchi hiyo wamekamatwa na kufikishwa kizimbani.

Taarifa iliyotolewa Jumatano imesema Jeshi la Thailand limesikitishwa na tukio la Disemba 16 ambapo raia watatu Waislamu walipigwa risasi na kuuawa katika tukio ambalo limedaiwa limefanyika 'kimakosa'.

Hayo yanajiri wakato ambao nchi ya Thailand, ambayo aghalabu ya wakazi wake wengine wanafuata dini ya Kibudhaa, imekuwa ikikabiliwa na uasi wa Waislamu  wanaotaka mamlaka ya kujitawala jimbo la Narathiwat kusini mwa nchi hiyo.

Takribani watu 7,000, wengi wakiwa ni raia , wameuawa katika uasi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda wa miaka 15 katika eneo hilo.

Kuna idadi kubwa ya wanajeshi katika eneo hilo huku kukiwa na mashambulizi ya kulipiza kisasi ambayo hutekelezwa na waasi baada ya misako ya vikosi vya usalama.

Kwa muda mrefu Waislamu wa Thailand wananyanyaswa katika nchi hiyo yenye Mabudha wengi.

3866499

Tags: iqna ، Waislamu ، Thailand
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: