IQNA

Misikiti nchini Thailand kuwakaribisha tena waumini

12:57 - September 07, 2021
Habari ID: 3474269
TEHRAN (IQNA) - Ofisi ya Sheikul Islam (SIO) nchini Thailand imeidhinisha kuanza kwa ibada kwenye misikiti katika jamii ambazo angalau 70% ya idadi ya watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi wamepewa chanjo dhidi ya COVID-19.

SIO ilitoa taarifa ikisema sasa inaruhusu Sala katika misikiti ya maeneo ambayo wakuu kamati za Kiislamu za mkoa na magavana wa mkoa kwa pamoja wameamua kupunguza vizuizi kwa shughuli za kidini.

Ofisi hiyo imesema ni lazima wajumbe wa kamati za Kiislam kwenye misikiti na waumini wawe wamepewa chanjo angalau mara moja. Aidha wakati wa Sala ni mfupi ambapo kwa Sala tano za siku ni dakika 30 kila Sala na Sala ya Ijumaa isizidi dakika 45.

Kulingana na Ofisi ya Sheikul Islam, wahudhuriaji Sala ni lazima wazingatie hatua za afya ya umma na tangazo la SIO. Wanatakiwa kupima joto la mwili wao kabla ya kuingia msikitini, kuvaa barakoa, na kuweka umbali wa mita 1.5 hadi 2 kati ya kila safu wakati wa Sala. Aidha vitakasafi mikono lazima vipatikane kwa urahisi.

Kulingana na ripoti ya mwaka 2007 ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Thailand kote Thailand kuna misikiti 3,494, ambapo misikiti 636 pekee iko katika Mkoa wa Pattani.

Waislamu wa Thailand ni kutoka mataifa na kaumi tofauti ambapo wengine wamehamia huko kutoka China, Pakistan, Cambodia, Bangladesh, Malaysia, na Indonesia, na vile vile kuna Waislamu wenyeji wa Thailand.

3995410

captcha