IQNA

11:21 - December 13, 2019
News ID: 3472274
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani vikali hatua ya utawala haramu wa Israel kukamata wanachama wake katika eneo inalolikalia kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel vimeendeleza chokochoko zake kwa kuwatia mbaroni viongozi kadhaa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) mjini al-Khalil (Hebron), katika Ukiongo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Shirika la habari la Ma’an la Palestina limeripoti kuwa, viongozi hao wa ngazi za juu wa HAMAS walikamatwa mapema jana Alkhamisi katika hujuma ya alfajiri ya askari wa utawala huo pandikizi.

HAMAS imethibitisha habari hiyo ya kukamatwa viongozi wake hao na kusema katika taarifa kuwa, kamatakamata na utekaji nyara ni katika mbinu zinazotumiwa na utawala wa Kizayuni, kwa shabaha ya kuvuruga siasa za ndani za Palestina.

Baadhi ya viongozi wa HAMAS waliotiwa nguvuni na askari wa Israel katika uvamizi huo wa jana mjini al-Khalil ni pamoja na aliyekuwa mbunge katika Baraza la Sheria la Palestina Muhammad Jamal al-Natshah, waziri wa zamani Issa al-Jabari, pamoja na Sheikh Abd al-Khaleq al-Natshah, Sheikh Jawad Bahr al-Natshah, Mazen al-Natshah, na Omar al-Qawasmi.

Haya yanajiri siku chache baada ya HAMAS kutahadharisha kuhusu vitendo vya walowezi wa Kizayuni vya kuendelea kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

HAMAS imeonya kuwa, njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kulazimisha matakwa yake kuhusiana na Msikiti wa Alqsa hazitazaa matunda na Intifadha na mapambano ya wakazi wote wa Quds ni ujumbe wa wazi kwa viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.

3470092/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: