IQNA

Rais Rouhani wa Iran atuma salamu za mwaka mpya wa 2020

10:11 - January 01, 2020
Habari ID: 3472323
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe wa pongezi marais na viongozi na mataifa ya Wakristo kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Miladia wa 2020.

Katika ujumbe wake wa mwaka mpya, Rais  Rouhani amesema, "Natumai kwamba, katika mwaka huu unaoanza, viongozi wa dunia wataimarisha ushirikiano wao na kusimama dhidi ya ubeberu, sambamba na kuchukua maamuzi ya kauli na vitendo kwa misingi ya sheria na uhuru, pamoja na kuufanya mpya huu uwe wa amani kwa wanadamu wote."

Rais Rouhani mbali na kuwatakia Wakristo duniani mwaka mpya wenye baraka, utulivu na amani amebainisha matumaini yake kuwa, viongozi wa dunia wataweza kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoyakabili mataifa yao.

Leo tarehe Mosi Januari inayosadifiana na kuanza mwaka mpya wa 2020 Miladia, ni siku kuadhimisha mwaka mpya katika jamii za Wakristo duniani.

Mpangilio wa miezi ya mwaka wa Kirumi unaoanza Januari hadi Disemba ulianza kutumiwa katika kipindi cha Mfalme Numa Pompilius yapata miaka 700 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa Masih AS. Kwa msingi huo tarehe 31 Disemba huwa siku ya mwisho ya mwaka wa Miladia na usiku wa kuamkia tarehe Mosi Januari huanza sherehe za kupokea mwaka mpya katika jamii za Wakristo na nchi nyingi za Afrika, America, Ulaya, Australia na hata Asia.

113059

captcha