IQNA

Rouhani:Marekani itashuhudia athari za jinai yake ya kumuua Luteni Jenerali Suleimani

14:17 - January 04, 2020
Habari ID: 3472334
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani amesema: Jina la Luteni Jenerali Qassem Soleimani litaheshimika na kubakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo mapema leo alipofika nyumbani kwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ili kuonana na familia ya shahidi huyo mtukufu, ambapo alitoa mkono wa hongera na wa pole kwa kuuawa kwake shahidi kwenye heshima kubwa.

Dakta Rouhani ameashiria jinai iliyofanywa na Marekani ya kumuua shahidi kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kwamba: Si leo hii tu, lakini katika miaka ijayo pia Marekani itashuhudia athari za hatua yake hiyo ya kijinai.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, hakuna shaka kuwa leo hii Marekani inachukiwa zaidi na wananchi wa Iran na Iraq; na akaongeza kwamba, huduma na mchango aliotoa Luteni Jenerali Soleimani kwa ajili ya kudhamini usalama wa Iran na eneo, na hasa kwa wananchi wa Iraq, Syria, Yemen, Lebanon na Afghanistan hAidha amesisitiza kuwa taifa la Iran lina haki isiyo na shaka na bila shaka litalipiza kisasi cha damu ya shahidi Qassem Soleimani na akabainisha kuwa, maadui walikasirishwa mno na hatua na mikakati ya Jenerali Soleimani ya kuimarisha uthabiti na usalama katika eneo na ndio maana wamemuua shahidi kidhulma na kikhabithi.

Amesisitiza pia kwamba Luteni Jenerali Soleimani hakuwa kamanda wa vita tu, lakini pia alikuwa mwanasiasa na mwanastratejia mwenye kipawa na asiye na mfano na akaongeza kwamba: "Vijana wa Iran wanafuata na wana mapenzi makubwa na njia ya shahidi Qassem Soleimani na kuna makumi ya Luteni Jenerali Soleimani ambao wanaandaliwa katika nchi hii".autasahaulika.

3868783

captcha