IQNA

21:56 - January 05, 2020
News ID: 3472338
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Mashia wa Iraq, Ayatullah Sayyed Ali al-Sistani amemtumia risala ya rambirambi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei kufuatia kuuawa shahidi kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Liteni Jenerali Qassem Soleimani.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni habari za kuuawa shahidi Jenerali Hajj Qassem Soleimani," Ayatollah Sistani ameandika katika ujumbe wake huo wa Jumapili.

Ayatollah Sistani ametuma salamu za rambi rambi kwa Kiongozi Muadhamu, familia ya Shahidi Soleimani, taifa la Iran na hasa watu wa mji wa Kerman alikozaliwa Shahidi Soleimani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq la Al-Hashdu-Sha'abi pamoja na watu wanane wengine waliuawa shahidi usiku wa manane wa kuamkia Ijumaa katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na majeshi vamizi na ya kigaidi ya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.

3869477/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: