IQNA

Ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa

22:16 - January 28, 2020
Habari ID: 3472414
TEHRAN (IQNA) – Vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa viliongezeka kwa asilimia 54 katika mwaka uliopita wa 2019.

Kwa mujibu wa ripoti ya wiki hii ya Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Vitendo vya Chuki dhidi ya Uislamu, kulikuwa na vitendo 100 vya hujuma dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa mwaka 2018 na idadi hiyo iliongezeka na kufika 154 mwaka uliopita wa 2019.

Katika taarifa, Abdallah Zekri, Rais wa Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Vitendo vya Chuki dhidi ya Uislamu, amesema vitendo hivyo vya kuwahujumu Waislamu vimeshuhudiwa zaidi katika maeneo ya  Ile-de-France, Rhones-Alpes na Paca nchini Ufaransa.

Huku akisisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote baina ya ugaidi na Uislamu amesema Waislamu nchini Ufaransa wanapaswa kuwa na haki ya kutekeleza mafundisho ya dini yao kwa uhuru kama wafuasi wa dini zingine nchini humo.

Hayo yanaripotiwa wakati ambao, Rais Macron amekuwa akitekeleza sera  kuzuia harakati za Waislamu nchini Ufaransa na kuwawekea mipaka kama vile kuzuia vazi la Hijabu kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Kiislamu. Hivi karibuni Ahmet Orgas, mkuu wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) alionya juu ya nia mbaya iliyo nyuma ya pazia ya Emmanuel Macron kuwalenga Waislamu.

Kuna takribani Waislamu milioni sita Ufaransa wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za kaskazini mwa Afrika na idadi hiyo ni takribani asilimia nane ya Wafaransa wote.

3470466

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha