IQNA

Asilimia 42 ya Waislamu Ufaransa wanabaguliwa

23:33 - November 07, 2019
Habari ID: 3472204
TEHRAN (IQNA) – Uchunguzi wa maoni umebaini kuwa asilimia 42 ya Waislamu Ufaransa wanabaguliwa au kubughudhiwa nchini humo.

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Maoni ya Umma Ufaransa umebaini kuwa Waislamu wanabaguliwa na kusumbuliwa bila sababu wakati wa doria ya polisi, wanapotaufta kazi na wanapokodi nyumba.

Asilimia 60 ya wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu au mtandio wanasema wamewahi kubaguliwa au kusumbuliwa kwa uchache mara moja.

Siku chache zilizopita pia, Jean-Luc Antoine Pierre Mélenchon, mwenyekiti wa chama cha La France Insoumise (Ufaransa Haisalimu Amri) alimtuhumu Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa kuchochea chuki dhidi ya Waislamu.

Mwanasiasa huyo, amesema kuwa tabia ya kuwatupia lawama Waislamu wa Ufaransa, inapasa kukomeshwa. Ufaransa ni nchi yenye jamii kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya, ambapo licha ya serikali ya Paris kujiepusha kutangaza takwimu rasmi za jamii ya Waislamu, nchi hiyo inakadiriwa kuwa na Waislamu milioni sita.

Haya yanaripotiwa siku chache baada ya ais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameendelea sera zake za chuki dhidi ya Uislamu kwa kusema anapinga vazi la staha la Hijabu la wanawake Waislamu kuvaliwa katika idara au taasisi za kiserikali zinazotoa huduma kwa umma. Akizungumza katika kisiwa cha Re Union Alhamisi, Macron amesema hajali iwapo wanawake Waislamu wanavaa hijabu katika sehemu za umma au hadharani lakini anapinga wafanyakazi wa idara au taasisi za kiserikali kuvaa Hijabu. Rais wa Ufaransa amesema hasa anapinga vazi la Hijabu katika shule za serikali.

Hivi karibuni Ahmet Orgas, mkuu wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) ameonya juu ya nia mbaya iliyo nyuma ya pazia ya Emmanuel Macron kuwalenga Waislamu.

3469823

Kishikizo: iqna ، Ufaransa ، Waislamu ، Ubaguzi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha