Bi. Abyar ametunukiwa zawai hiyo na Shirika la HUM la Pakistan ambalo hujishughulisha na masuala ya habari na lina baadhi ya televisehni kubwa zaidi katika nchi hiyo.
Abyar ameshinda zawadi kadhaa za kitaifa na kimataifa kutokana na kazi yake ya utegenejzaji filamu. Zawadi ambayo Bi. Abyar ametunukiwa hutunukiwa wanawake ambao wameweza kupata mafanikio makubwa katika nchi mbali mbali duniani
Sherehe za kuwatunuku zawadi washindi wa mwaka huu zimefanyika katika mji wa Karachi Jumatano na kuhudhuriwa na Rais wa Pakistan Dkt. Arif Alvi na wageni wengin. Washindi wngine walikuwa ni Omer Aftab, Khadija Siddiqi, Dr Seemin Jamali, Dr Shamshad Akhtar, Jalila Haider, Maleeha Lodhi na Mary Robinson kutokana na kazi zao katika nyuga wanazojishughulisha nazo.