IQNA

Imam wa Ahlul Sunna mjini Zahedan, Iran

Ushauri wa Mtume SAW kuhusu kukabiliana na magonjwa ambukizi

12:09 - February 23, 2020
1
Habari ID: 3472498
TEHRAN (IQNA) - Imam wa Ahul Sunna katika mji wa Zahedan, kusini mashariki mwa Iran ameashiria kuenea virusi vya Corona na kusema Mtume Muhammad SAW alitoa nasaha kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwa ambukizi ya tauni na kipindupindu.

Molavi Abdol-Hamid Ismail-Zahi, Imam wa Sala ya Ijumaa wa Ahul Sunna katika mji wa Zahedan ameashiria Hadithi ya Mtume Mtukufu alisema  wakati ugonjwa wa tauni unapoenea katika eneo, wakaazi hawapaswi kuondoka eneo hilo na wengine hawapaswi kuingia katika eneo hilo kwani kufanya hivyo kutapelekea ugonjwa huo kuenea zaidi.

Akihutubia wanafunzi leo katika Chuo cha Darul Uluum mjini Zahedan amesema: "Uislamu si dini ya nadharia bali ni dini ya vitendo."

Aidha amesema Sira ya Mtume SAW ina uwezo mkubwa wa kutumia katika maisha.

Akizungumzia kirusi cha  Corona amesema: "Imearifiwa kuwa kirusi cha Corona pia kimefika katika nchi yetu na baadhi wameambukizwa katika baadhi ya mikoa." Molavi Abdol-Hamid IsmaIl-Zahi ametoa wito wa kutekelezwa ushauri wa Mtume SAW kuhusu magonjwa ambukuzi na pia amewataka wananchi wasiingiwe na hofu kubwa na watawakali kwa Mwenyezi Mungu SWT.

3880747

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
abdul mdoe
0
1
wakaazi hawapaswi kuondoka eneo hilo na wengine hawapaswi kuingia katika eneo hilo kwani kufanya hivyo kutapelekea ugonjwa huo kuenea zaidi. kurasa number ngapi cha qurqn
captcha