IQNA

11:59 - March 09, 2020
News ID: 3472548
TEHRAN (IQNA) - Vyombo vya habari vya Ufaransa vimetangaza kuwa, jana usiku mtu mmoja mwenye silaha alishambulia msikiti mmoja mjini Parisa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ufaransa, gaidi huyo mwenye silaha aliwashambulia kwa risasi Waislamu msikitini katika eneo la Rue de Tanger, mjini Paris.

Muislamu mmoja amejeruhiwa kwenye shambulio hilo la kigaidi. Polisi wa eneo hilo wamepata risasi sita katika eneo la tukio. Vyombo hivyo vya habari vya Ufaransa vimesema, gaidi aliyefanya shambulizi hilo dhidi ya Waislamu ametoroka na hajulikani alipo. Ufaransa imeshuhudia matukio mengi ya kushambuliwa misikiti na Waislamu katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Hadi hivi sasa Waislamu wa Ufaransa wameshawasilisha malalamiko yao kwa vyombo husika kulalamikia vitendo vya kigaidi na chuki za kidini wanazofanyiwa nchini humo wakivitaka viimarishe ulinzi hasa katika maeneo ya ibada ya Waislamu.

Maadui wa Uislamu wamekuwa wakieneza chuki kubwa dhidi ya Waislamu barani Ulaya hasa huko Ufaransa kutokana na vitendo vya kigaidi vya magenge yaliyotengenezwa na nchi hizo hizo za Magharibi kama vile ISIS kwa lengo la kuupaka matope Uislamu.

Wataalamu na viongozi wenyewe wa nchi za Magharibi wamekiri kwamba sababu kuu ya machafuko barani humo ni uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa magenge ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq.

Taarifa zinasema kuwa, mamia ya magaidi wenye asili ya Ufaransa wanapigana bega kwa bega na magaidi wengine hivi sasa huko Idlib, Syria.

3470860

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: