IQNA

21:40 - March 27, 2020
News ID: 3472607
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ameambukizwa ugonjwa hatari wa COVID-19 au corona unaoenea kwa kasi kubwa dunia nzima.

Johnson amenukuliwa akisema katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa amekumbwa na ugonjwa hatari wa COVID-19. 

Vile vile amesema kuwa atajiweka kwenye karantini nyumbani. Aidha Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock naye pia ameambukizwa corona.

Huku hayo yakiripotiwa, kasi ya maambukizi na vifo vitokanavyo na corona nchini Uingereza imeongezeka sana kiasi kwamba katika kila dakika 13 mtu mmoja anafariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 Uingereza.

Mtandao wa Intaneti wa gazeti la Mirror umeripoti habari hiyo leo Ijumaa na kuzinukuu duru za hospitali zikisema kuwa, katika kila dakika 13 mtu mmoja anafariki dunia hivi sasa kutokana na kirusi cha corona huko Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hivi sasa wagonjwa 4300 wamelazwa hospitalini nchini humo kutokana na ugonjwa wa corona 578 wameshafariki dunia huku watu 11,658 wakiwa wameshaambukizwa kirusi hicho kulingana na taarifa rasmi ambazo baadhi ya mashuhuda wanasema idadi ya waathiriwa ni kubwa zaidi ya hiyo inayotangazwa na serikali ya Uingereza.

3887690

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: