IQNA

Iran yatahadharisha
9:50 - April 02, 2020
News ID: 3472625
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria harakati za wanajeshi wa Marekani huko Iraq na kueleza kuwa, harakati hizo mbali na kukiuka mamlaka ya kitaifa ya Iraq zinasababisha ghasia na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi.

Sayyid Abbas Mousavi amesisistiza kuwa harakati za karibuni za kijeshi za wanajeshi wa Marekani huko Iraq ni kinyume na takwa la Serikali, wananchi na Bunge la nchi hiyo. 

Katika siku chache za hivi karibuni kuwekuwepo operesheni kabambe ya kuhamishwa wanajeshi wa Marekani kutoka sehemu moja ya kupelekwa jingine ndani ya ardhi ya Iraq.

Baadhi ya ripoti zinazitaja harakati hizo mpya za wanajeshi wa Marekani huko Iraq kuwa zinahusiana na njama ya mapinduzi na kwamba ni mashinikizo kwa lengo la kubadili mchakato wa kisiasa nchini Iraq kwa maslahi ya siasa za Marekani.  

Shirika la habari la Ufaransa Jumatatu usiku lilifichua kuwa Marekani imetuma ngao ya makombora ya Patriot katika kambi zake za jeshi huko Erbil na Ain al Asad mkoani al Anbar huko Iraq. Wakati huo huo baadhi ya wakuu wa makundi ya muqawama wa Kiislamu ya Iraq wamtangaza kuwa hawatakaa kimya mbele ya hatua hizo zenye kutia shaka za Marekani na watajibu hatua hizo. 

3888532

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: