Yasser Abdul Zahra Al-Hajjaj alitoa kauli hizo katika mahojiano na IQNA mjini Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran alikofika kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Hadhi ya Binadamu na Changamoto za Familia katika Ulimwengu wa Kisasa.
"Msingi wa kukuza utu wa binadamu na haki za kimsingi zinazohusiana, pamoja na haki za binadamu kwa ujumla, ni utamaduni," alisema. "Jamii inaposonga mbele kuelekea maadili ya kitamaduni, utu wa binadamu pia hufikia kiwango kinachohitajika. Kwa hivyo, kuna uhusiano wa maana kati ya hizo mbili."
Uhusiano wa Iran na Iraq
Akizungumzia uhusiano wa kipekee kati ya Iran na Iraq, Abdul Zahra aliangazia mafungamano ya kitamaduni hususan ya kidini na kiroho.
"Leo, tunapozungumza juu ya uhusiano kati ya Iran na Iraqi, tunazungumza juu ya uhusiano uliowekwa katika nyanja za kitamaduni. Iwapo tutazingatia mwelekeo mmoja tu wa mahusiano haya ya kitamaduni, kama vile mambo ya kidini, inatubainikia wazi kwamba mataifa haya mawili yanaenda katika mwelekeo wenye uwiano na mshikamano,” alibainisha.
Abdul Zahra alisisitiza umuhimu wa ziyara au matembezi kila mwaka ya Arbaeen kama tukio muhimu la kitamaduni na kijamii, linalovuka nyanja zake za kidini. "Arbaeen, kabla ya kuwa jambo la kidini, ni la kitamaduni na kijamii. Hali hii inaweza kusaidia mataifa yote mawili katika kuimarisha uhusiano wao,” alisema. "Kwa maneno mengine, msingi wa uhusiano wa Iran na Iraq ni wa kitamaduni, na moja ya viashiria vikali vya kipengele hiki cha kitamaduni ni dini."
Kongamano hilo la siku tatu limekamilika leo.
4247761