IQNA

Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri

Marekani itakabiliwa na jibu kali ikiteteresha usalama wa Iran

18:45 - April 02, 2020
Habari ID: 3472626
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Iran ameashiria harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kueleza kuwa Marekani itakabiliwa na jibu kali iwapo itachua hatua au kutaka kuteteresha usalama wa Iran.

Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu na majeshi yake yote vinasimamia kwa makini maeneo yote ya mipaka ya nchi kavu, anga na baharini na kufuatilia kikamilifu harakati zote. 

Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa harakati za kijeshi za Marekani huko Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi zinapigiwa debe na makelele mengi katika vyombo vya habari vya vibaraka wa Marekani dhidi ya wanamuqawama huko  Iraq na kikosi cha wapiganaji wa kujitolea cha wananchi cha al Hashd al Shaabi. 

Brigedia Baqeri Baqeri amesisitiza kuwa viongozi wa Marekani wanafahamu vyema kwamba wananchi wa eneo hili wakiwemo wa Iraq wanapinga kuweko majeshi ya nchi hiyo katika nchi hizo.  

Harakati za kijeshi zinazotia shaka za Marekani za kuwahamisha wanajeshi wake huko Iraq sambamba na ripoti zinazosema kuwa Washington inafanya mipango ya kuyashambulia baadhi ya makundi ya muqawama wa Kiislamu na lile la al Hashd al Shaabi, vimeibua wasiwasi ncini Iraq.

3888680

captcha