IQNA

21:58 - May 19, 2020
News ID: 3472781
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) utafunguliwa kwa waumini baada ya siku kuu ya Idul Fitr.

Kwa mujibu wa Bodi ya Usimamizi wa Al-Aqsa, msikiti huo utafunguliwa baada ya kufungwa kwa muda wa miezi miwili ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Taarifa hiyo imesema tarehe hasa ya kufunguliwa msikiti huo itatangazwa baadaye.

Al-Aqsa ni Msikiti wa tatu kwa utakatifu katika Uislamu baada ya Misikiti Miwili Mitakatifu (Haramein) ya Makka na Madina ambayo nayo pia imefungwa kwa muda kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha corona.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama zake za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Quds

Uvamizi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina.

3471477

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: