IQNA

10:30 - May 21, 2020
News ID: 3472787
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameutahadharisah vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuchukua hatua zozote dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).

Kiongozi wa Idara ya Kisiasa ya Hamas, Ismail Haniya ameyasema hayo Jumatano katika hotuba aliyotoa kwa kwa njia ya video kwa mnasaba wa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds.

Aidha amesema "Muamala wa Karne" unakusudia kusambaratisha kadhia ya Palestina.

Haniyah ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kufanya jinai na kuchukua hatua yoyote ya kipumbavu.

Haniya amesisitiza pia kuwa, muqawama na mapambano ya wananchi madhulumu wa Palestina yataendelea mpaka pale yatakapopata ushindi dhidi ya Wazayuni na kuongeza kuwa, Quds hivi sasa inakabiliwa na vitisho vingi na ipo katika hatari ya kuyahudishwa na kubadilishwa.

Kiongozi wa Hamas aidha ameishukuru kwa dhati Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono mapambano ya Palestina na kusema uungaji mkono huo wa Iran ni stratijia iliyowekwa na Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu), Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha amesema hatua ya Imam Khomeini (MA) kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni jambo ambalo liliupa uhai mpya muqawama na mapabano ya kupigania ukombozi wa Palestina.

3900454

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: