IQNA

Askari wa utawala wa Israel wawahujumu waumini katika Swala ya Idul Fitr

12:06 - May 24, 2020
Habari ID: 3472796
TEHRAN (IQNA) - Wanjeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina waliokuwa wamefika katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) kwa lengo la kushiriki katika Swala ya Idul Fitr.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Safa la Palestina, wanajeshi wa utawala bandia wa Israel mapema leo asubuhi waliwashambulia Wapalestina hao kwa marungu na nyuti za bunduki ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Wapalestina hao walikuwa wamefika maeneo ya karibu na Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Swala ya Idi.

Makumi ya waumini waliokusanyika walijaribu kuvua vizingiti vya chuma vilivyowekwa na utawala ghasibu wa Israel na hapo makabiliano yakaanza na askari wa utawala huo. Wapalestina hao hatimaye waliweza kuswali Swala ya Idu katika Medani ya Al Ghazala katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika lango la Babul Asbaat la msikiti huo.

Wakiwa hapo waliweza kusikiliza hotuba ya Swala ya Idi ambayo ilikuwa ikisikika ndani ya Msikiti wa Al Aqsa. Eneo la ndani la Msikiti wa Al Aqsa limefungwa kwa muda wa miezi miwili sasa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19  na kwa mujibu wa Idara ya Wakfu Palestina, msikiti huo utafunguliwa kikamilifu baada baada ya siku kuu ya Idul Fitr.

3901129/

captcha