IQNA

12:31 - May 29, 2020
News ID: 3472813
TEHRAN (IQNA) - Serikali ya Syria imemfungua tena Haram Takatifu ya Bibi Zainab (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake -SA-) katika kiunga cha mji mkuu, Damascus, miezi miwili baada ya kufungwa.

Kwa mujibu wa taarifa, idadi kubwa ya wafanyaziara wameanza kumiminika katika eneo hilo takatifu ambalo lilifungwa Mwezi Machi kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Kamati inayosimamia Haram ya Bibi Zainab SA awali ilikuw aimesema eneo hilo litafungwa hadi Aprili 2 lakini muda wa kufungwa kwake uliongozwa.
Wizara ya Afya ya Syria imesema hatua ya kufunga harama hiyo tayakiifu ilichukuliwa kwa lengo la kulinda afya ya wafanyaziara.
Bbi Zainab (SA) binti mtukufu wa Imam Ali bin Abi Twalib (AS) na Bibi Fatimatu Zahraa (AS). Bibi Zainab alikuwa mashuhuri miongoni mwa watu kutokana na maarifa na elimu kubwa aliyokuwa nayo. Katika tukio la Karbala, Bibi Zainab (SA) alisimama kidete na kukabiliana na dhulma za watawala dhalimu na ujahili watu wa zama hizo ili kutimiza malengo matukufu ya kaka yake, Imam Hussein (AS). Bibi Zainab alipelekwa Sham pamoja na mateka wengine wa Nyumba Tukufu ya Mtume (saw) baada ya mapambano ya Imam Hussein (AS) huko Karbala. Hotuba za Bibi Zainab mbele ya majlisi ya Ibn Ziyad mtawala wa Kufa na katika ikulu ya Yazid bin Muawiya huko Sham zilikuwa na taathira kubwa katika kufichua dhulma na ukandamizaji wa Bani Umayya na kuonesha jinsi Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume walivyodhulumiwa.

3901722

بازگشایی حرم حضرت زینب(س) + عکس

بازگشایی حرم حضرت زینب(س) + عکس

بازگشایی حرم حضرت زینب(س) + عکس

Tags: syria ، bibi Zainab ، COVID-19
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: