IQNA

21:46 - June 20, 2020
News ID: 3472881
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimelaani matamshi ya mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Austria ambaye alivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Katika taarifa Idara ya Al Azhar ya Kufuatialia Vitendo vya  Chuki dhidi ya Uislamu imelaani vikali uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu ambao unazidisha migawanyiko katika jamii.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, matamshi kama hayo yanawachochea hujuma za kigaidi dhidi ya Waislamu.

Mwanachama wa chama cha mrengo wa kulia cha Austria (FPO) Horbert Hofer akihutubu katika mkutano wa kisiasa Jumanne alidai kuwa Qur’ani Tukufu “ni hatari zaidi ya kirusi cha corona’. Matamshi hayo yamekosolewa vikali na chama Social Democrat cha Austria na pia Jumuiya ya Kiislamu ya Austria (IGGO).

Waislamu nchini Austria wamesema watawasilisha malalamiko rasmi dhidi ya mwanasiasa huyo mchochezi. Mwenyekiti IGGO Umit Vural amesema Hofer amewatusi Waislamu wote kwa matamshi yake.

3905593

 

 

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: