IQNA

17:49 - June 21, 2020
News ID: 3472883
TEHRAN (IQNA) - Leo Jumapili mamilioni ya watu katika mabara ya Afrika, Asia na Ulaya wameshuhudia moja ya tukio la jua kupatwa na mwezi.

Hapa nchini Iran tukio hilo limejiri katika mji mkuu Tehran na pia katika miji mingine na wengi wameshuhudia tukio hilo kwa kuvaa miwani maalumu. Tukio hilo la kupatwa jua mjini Tehran limeanza saa tatu na dakika nne hadi saa tano na dakika 3 asubuhi. Katika ukanda wote wa Afrika Mashariki pia tukuo hilo limeshuhudiwa na wengi mapema leo asubuhi.

Kupatwa kwa Jua (kwa Kiingereza solar eclipse) ni hali ya jua kutoonekana (au kuonekana kwa sehemu tu) angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo mawingu. Kunatokea wakati mwezi unapita kati ya jua na dunia na kufunika jua. Tokeo lake ni kupungua kwa nuru ya jua hadi kutoonekana kwa muda wa kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu. Katika tukio la leo jua limefunikwa kabisa katika maeneo machache tu huku maeneo mengi ya kishuhudia kufunikwa sehemu ya jua.

Kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, wakati tukio kama hili la kupatwa jua linapojiri,  waumini wanatakiwa kuswali swala maalumu inayojulikana kama Swalatul Ayaat au swalatu kusuf.

Marajii wa Kishia wanasema ni wajibu kuswali Swalatu Ayaat wakati wa kupatwa jua hata kama muumini hajashuhudia tukio hilo kwa macho yake.

Wakati huo huo, katika kikao cha leo asubuhi cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, mjini Tehran, wabunge walisitisha kikao chao kwa muda wa dakika 20 asubuh ili kuswali Swalatul Ayaat.

3906081

Tags: kupatwa jua ، mwezi
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: