IQNA

22:27 - July 01, 2020
News ID: 3472918
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Algeria amekataa kuafiki mapendekezo ya kufungua misikiti nchini humo kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini humo.

Abdelaziz Djerad amesema  kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya na madaktari, haiwezekani kufungua misikiti ya nchi hiyo ambayo ilifunguwa mwezi Machi ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

“Pundu ugonjwa wa corona utakapoangamizwa, basi sote tutaswali pamoja swala ya jamaa katika misikiti,” amesema Waziri Mkuu Dejrad.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na miito ya kutaka misikiti ifunguliwe.

Hadi kufikia sasa watu 14,272 wameambukizwa corona nchini Algeria huku wengine 920 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo unaozidia kuenea kwa kasi kote duniani.

/3471851

Tags: algeria ، misikiti ، COVID-19
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: