IQNA

Matembezi ya Arobaini ya Imam Hussein AS katika barabara ya Basra-Karbala

TEHRAN (IQNA) - Kama miaka iliyopita, Waislamu, aghalabu wakiwa ni wa madhehebu ya Shia, wameanza matembezi ya kuelekea katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya maadhimisho ya Arobaini ya Iman Hussein AS.

Majlisi na matembezi ya siku ya Arobaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.