Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Imam Hussein (AS) umepangwa kufanyika Machi mwaka huu, ukiandaliwa na Kituo cha Dar ul-Quran cha Haram Takatifu wa Imam Hussein (AS) kama sehemu ya shughuli za Siku ya Kimataifa ya Qur’ani huko Karbala.
Katika muktadha huu, ujumbe kutoka Dar ul Quran ulisafiri kwenda mji mtakatifu wa Najaf kushauriana na kujadili na wanazuoni wa Seminari ya Najaf.
Nadhir al-Dalfi, mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari vya Quran katika Haram ya Imam Hussein (AS), alisema, "Wakati wa ziara hii, ujumbe wa Dar al-Quran ulikutana na viongozi kadhaa wa kidini na wanazuoni kutoka Seminari ya Najaf kujadili njia za kuhakikisha mafanikio ya mkutano huo na kuufanya katika kiwango kinachostahili hadhi ya Imam Hussein (AS) na ujumbe wake wa kiutu wa kimataifa."
Aliongeza, "Mkutano huu ni sehemu ya juhudi za Dar ul-Quran za kuunganisha juhudi za pamoja na kuangazia athari za Qur’an na fikra za harakati za Imam Hussein (AS)."
"Dar ul-Quran inalenga kufanya mkutano huu kuwa jukwaa la kimataifa la kuelimisha watu kuhusu maadili ya kibinadamu na ya imani ya shule ya Imam Hussein," alisisitiza.
349140