Eneo hilo ambalo ni maarufu la Bain-ul-Haramain, kati ya maziara haya mawili , imekuwa kitovu cha shughuli hizi za kihistoria na kiroho.
Makundi ya waombolezaji, kwa kufuata mila ya kale ya maombolezo, hutembelea maeneo hayo matakatifu ili kufanya maombolezo na kuendeleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS ambaye pia ni Imam wa Tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia pamoja na maswahaba wake waaminifu waliotoa maisha yao kwa ajili ya haki.
Shughuli hizi zinafanyika chini ya mpango ulioratibiwa kwa umakini na Idara ya Maombolezo na Maandamano ya Husseini chini ya usimamizi wa Idara za Wafawidhi wa maeneo hayo matukufu, na zitaendelea katika kipindi chote cha mwezi wa Muharram.
Makundi haya ya waombolezaji, kwa kufuata njia zilizopangwa tayari, huanza kutoka mlango wa Bab al-Qiblah wa ziara ya Hazrat Abbas (AS), ambapo huendesha sehemu ya ibada katika uwanja wa haram hiyo. Kisha hupita njia ya Bain-ul-Haramain kuelekea kwenye ziara ya Imam Hussein (AS) ambako hufunga maombolezo yao.
Ili kuhakikisha mpangilio na utulivu wa hafla hizo, Idara ya Maombolezo huandaa vikosi maalum vya kusimamia kila msafara tangu mwanzo hadi mwisho wake, kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa utaratibu bila kuvuruga harakati za mahujaji wengine.
Waislamu wa madhehebu ya Shia, na wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani, huadhimisha kila mwaka mwezi wa Muharram kwa kufanya maombolezo ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS) na wafuasi wake.
Imam Hussein (AS), aliyekuwa mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), pamoja na jamaa na maswahaba wachache waaminifu, waliuawa shahidi na mnyanyasaji wa wakati huo Yazid bin Muawiya, katika vita vya Karbala mnamo siku ya kumi ya Muharram (Ashura), mwaka wa 61 Hijria sawa 680 Miladia.
Maombolezo haya ni ukumbusho wa mapambano ya haki dhidi ya dhulma na dhihirisho la mapenzi ya kweli kwa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul Bayt).
4291306