IQNA

Wanachama Waislamu: Kuna chuki dhidi ya Uislamu katika Chama cha Leba Uingereza

22:26 - November 15, 2020
Habari ID: 3473362
TEHRAN (IQNA) – Wanachama Waislamu katika chama cha Leba cha Uingereza wamesema wameshuhudia chuki dhidi ya Uislamu katika chama hicho kikubwa zaidi Uingereza.

Uchunguzi uliotanywa na Mtandao wa Waislamu Katika Leba umebaini kuwa zaidi ya asilimiA 33 ya Waislamu wanaofungamana na Chama cha Leba wameshuhudia chuki dhidi ya Uislamu katika chama hicho.

Aidha uchunguzi umebaini kuwa asilimia 44 ya wanachama hao wanaamini kuwa chama cha Leba halilipi uzito unaostahiki suala la chuki dhidi ya Uislamu huku asilimia 48 wakisema hawana imani tena na muundo wa kuwasilisha malalmiko katika chama.

Ali Reza Milani ambaye alikuwa mpizani wa waziri mkuu Boris Johnsen katika eneo bunge la Uxbridge and South Ruislip katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana amesema kuwa wanachama wenza walimuambia kuwa Waislamu hawapaswi kuwa bunge kutokana na ‘kuegemea katika utumiaji mabavu’ huku baadhi wakimuuliza iwapo  yeye ni gaidi. Anasema aliumizwa sana na matamshi hayo na hata baada ya malalmiko ilichukua mwaka mmoja kabla ya chama kuwasiliana naye kuhusu kadhia hiyo. Mbunge Muislamu kutoka Manchester Gorton, Afzal Khan, ambaye pia ni mwenyekiti wa Mtandao wa Waislamu katika Leba bungeni amesema kuna upuuzaji kuhusu uwepo wa chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia katika chama cha Leba ambacho kimekuwa kikiungwa mkono na Waislamu kwa miongo kadhaa.

Kiongozi wa Chama cha Leba Keir Starmer na naibu wake Angela Rayner wamesema: “Tunaushukuru Mtandao wa Waislamu katika Leba” kwa ripoti hii muhimu pamoja na jitihada zao za kuhakikisha kuwa wanachama Waislamu wanasikika.” Aidha wameongeza kuwa, “chuki dhidi ya Uislamu haina nafasi katika jamii yetu.”

3473120/

captcha