IQNA

Mbunge wa upinzani Uingereza muungaji mkono Wapalestina auawa

22:26 - June 17, 2016
Habari ID: 3470393
Mbunge wa chama cha upinzani cha Leba Uingereza, Bi. Jo Cox na ambaye alikuwa muungaji mkono Wapalestina amepigwa risasi na kuuawa.

Mbunge wa chama cha upinzani cha Leba Uingereza, Bi. Jo Cox na ambaye alikuwa muungaji mkono Wapalestina amepigwa risasi na kuuawa

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jo Cox aliyekuwa mbunge wa chama cha Labour, amefariki dunia kutokana na majeraha makali aliyopata baada ya kupigwa risasi Alkhamisi

Polisi ya Uingereza imemtia nguvuni bwana mmoja mwenye umri wa miaka 52 kwa tuhuma za kutekeleza kitendo hicho cha kigaidi.

Jo Cox alipigwa risasi na kudungwa kisu alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Birstall huko kaskazini mwa Uingereza.

Bi Cox alikuwa miongoni mwa wabunge wanaounga mkono suala la Uingereza kubakia katika Umoja wa Ulaya na ameuawa wiki moja tu kabla ya kura muhimu ya maoni ya kuamua iwapo nchi hiyo utabakia katika umoja huo au la. Vilevile Cox alikuwa muungaji mkono mkubwa wa Wapalestina na suala la kukaribishwa wakimbizi hususan watoto kutoka Syria nchini Uingereza.

3507748

captcha