IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Zahra Abbasi anaiwakilisha Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jordan

14:47 - February 17, 2024
Habari ID: 3478368
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya 18 ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake ya Jordan yatang'oa nanga katika mji mkuu Amman baadaye leo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa nchi zilizotuma wawakilishi katika mashindano hayo. Zahra Abbasi, aliyehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na ambaye anasoma lugha ya Kiarabu na fasihi katika Chuo Kikuu cha Tehran, anaiwakilisha Iran katika tukio la Qur'ani.
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Al-Hashimiya yataendelea hadi Februari 22, kwa mujibu wa Ali al-Daqamisa, msemaji wa wizara ya Awqaf ya Jordan.
Washindi watatajwa na kutuzwa katika hafla ya kufunga Alhamisi, alibainisha.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Wakfu ya Jordan kwa kushirikisha wahifadhi wanawake wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.
Mwaka jana, Roya Fazaeli aliiwakilisha Iran katika toleo la 17 na hakupata cheo licha ya utayari wake wa juu.
 
4200123

captcha