IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wanawake kutoka Nchi 39 Washiriki Mashindano ya Qur’ani nchini Jordan

19:50 - February 18, 2024
Habari ID: 3478372
IQNA – Toleo la 18 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Jordan kwa wanawake, yanayojulikana kama "Al-Hashimiya", yalianza Jumamosi huko Amman.

Hafla hiyo ambayo hufanyika kila mwaka huwandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan,na  mwaka hii inawashirikisha wahifadhi Qur’ani wanawake 41 kutoka nchi 39 mbalimbali.

Sherehe za ufunguzi zilihudhuriwa na Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Jordan, Mohammad Ahmad Muslim Al Khalayleh, ambaye alisisitiza umuhimu wa Qur'ani kama chanzo cha mwongozo, hekima, na mafanikio katika maisha.

"Katika ulimwengu huu, tuna hitaji kubwa la Qur’ani, ambayo inatuongoza katika njia sahihi na inatufundisha jinsi ya kufanya kazi, kufikiria, na kupata mafanikio na ushindi katika maisha yetu," alisema.

Yakishirikisha kategoria za hifdhi na quraa, mashindan hayo o ya Qur'ani yataendelea hadi Februari 22, washindi watakapotangazwa na kutunukiwa katika sherehe za kufunga.

Mwakilishi wa Iran katika mashindano hayo ni Zahra Abbasi, mwanafunzi wa lugha ya Kiarabu na fasihi katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambaye amehifadhi Qur'ani nzima.

3487235

captcha