Katika taarifa Alhamisi, Hizbullah immemtaja Sadiq al-Mahdi kuwa mwanasiasa aliyeheshimika kutokana na msimamo wake wa kupambamna na kupinga mabeberu wa kimataifa.
Al-Mahadi alifariki juzi baada ya kuambukizwa corona kwa muda wa iki tatu. Al-Mahdi, 84, alikuwa waziri mkuu wa mwisho kuchaguliwa kidemokrasia na alipinduliwa mwaka 1989 katika mapinduzi ya kijeshi yaliyomleta madarakani rais wa zamani Omar al-Bashir ambaye naye pia alipinduliwa na jeshi mwaka 2019.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, nayo pia imetuma salamu za rambi rambi kufuatia kuga dunia al-Mhadi na kumtaja kuwa muungaji mkono wa haki za Wapalestina.