IQNA

Sheikh Naeem Qassem

Kipumbele cha Marekani ni kulinda maslahi ya Israel Asia Magharibi

17:33 - February 05, 2021
Habari ID: 3473622
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Naeem Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kipaumbele cha serikali ya Marekani ni kulinda maslahi ya utawala haramu wa Israel katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati)

Katika mahojiano na Radio an-Noor, Sheikh Naeem Qassem amesema mazungumzo na serikali ya Marekani hayana maana.

Akitoa tathmini yake kuhusu mazungumzo tarajiwa ya Marekani na Iran kuhusu kadhia ya nyuklia,  amesema iwapo Marekani itarejea katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, basi Iran inayo itaanza kutekeleza ahadi zake katika mapatano hayo. Amesema yamkini hali ikatulia kuhusiana na kadhia ya nyuklia ya Iran lakini hakuna utatuzi wa haraka utakaopatikana.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema Hizbullah inakerwa na jambo moja tu muhimu nalo ni uwepo wa Wazayuni maghasibu katika eneo. Ameongeza kuwa,  katika mazungumzo yoyote tayarajiwa na Marekani na Wazayuni,  serikali ya Marekani itauunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia ardhi za wengine kwa mabavu.

Sheikh Naeem Qassim ameongeza kuwa, Wazayuni daima wako katika hali ya kuhujumu lakini mhimili wa muqawama unalenga kulinda mamlaka ya kujitawala na uhuru wa Lebanon. Ameongeza kuwa Hizbullah inazuia utawala wa Kizayuni wa Israel usivamie Lebanon.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah aidha amesisitiza kuhusu kuundwa serikali mpya nchini Lebanon na kuongeza kuwa, watu wa Lebanon wanataka serikali iundwe haraka iwezekanavyo na hivyo wote wanapaswa kuhitajidi kuhakikisha kuwa serikali shirikishi inaundwa.

3952194/

captcha