IQNA

Kongamano la Bima ya Kiislamu lafanyika Gambia

22:20 - December 05, 2020
Habari ID: 3473425
TEHRAN (IQNA) – Warsha kuhusu bima ya Kiislamu, inayojulikana kama Takaful, imefanyika hivi karibuni nchini Gambia.

Warsha hiyo imeandaliwa na shirika la West Africa Takaful kwa lengo la kuwailimisha washiriki kuhusu bima hiyo ya Kiislamu.

Shirika la West Africa Takaful lilianzishwa mwaka 2018 na limezidi kujiimarisha katika sekta ya bima ya Kiislamu nchini Gambia.

Momodou M. Joof, mkurugenzi wa West Africa Takaful  anasema wakati alipowasilisha fikra ya bima ya Kiislamu, vijana wengi wataalamu na wafanya biashara walikumbatia wazo lake baada ya muda mfupi.

Akizungumza katika kikao hicho, mwakilishi wa Benki Kuu ya Ghana Pa Alieu Silah amesema West Africa Takaful hutilia maanani zaidi msingi  wa uwezo wa wateja badala ya kujikita katika kupata faida tu.  Amesema sekta ya Takaful imestawi vizuri nchini Gambia katika kipindi cha miaka 12 tokea ianze shughuli zake nchini humo.

Kati ya mambo mengine, bima ya takaful haitegemei riba na gharar na hivyo inafungamana na mafundisho ya Kiislamu.

3938919

Kishikizo: takaful gambia bima
captcha