IQNA

Wanawake na Qur'ani

Kongamano la Qur'ani la Wanawake na Wasichana Gambia

16:09 - June 01, 2022
Habari ID: 3475321
TEHRAN (IQNA) - Kongamano la kila mwaka la Qur’ani la Jumuiya ya Qur’ani ya Wanawake na Wasichana ya Gambia liliandaliwa ili kukuza vipaji vya kielimu miongoni mwa wanachama wa jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Daara Aisha Ummul Mu’mineen (DAUM) kwa ajili ya Wasichana na Wanawake hivi karibuni iliandaa kikao cha kila mwaka cha usomaji Qur'ani Tukufu na kongamano ukumbi wa Baraza Kuu la Kiislamu la Gambia (GSIC).

Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Elimu na Maendeleo (IIED), ambayo chini ya asasi yake ya DAUM ilianzishwa, Sheikh Omar Ceesay alibainisha sifa za tukio hilo kuwa ni uwezeshaji kupitia elimu.

"Sehemu ya sababu za shughuli hii ni kuwahamasisha wanachama wa jumuiya ya wanawake juu ya jitihada zao za kujifunza na kubadilishana ujuzi wa Qur'ani na matendo ya Mtume mpendwa wa Uislamu. Hii pia ni kuwahakikishia wazazi au walezi na waume wanaowaruhusu wasichana na wanawake wao kujiunga na DAUM kwamba juhudi zao si za bure.”

Kawey Njie-Lette, mwenyekiti wa DAUM, alisema jumuiya hiyo inajumuisha wanafunzi wa kike wa rika zote na wa tabaka mbalimbali wakiwemo wale wa sekta ya umma na binafsi.

"Wanachama wetu wanatoka katika matabaka yote kijamii na miongoni mwetu ni wanafunzi, akina mama wakiwemo wale ambao mifano ya kuigwa walioungana katika kutafuta maarifa ili kuifanya jamii iwe mahala bora zaidi kwa maisha ya binadamu." alisema.

Alibaini kuwa wanawake ni akina mama ambao jamii haiwezi ishi bila wao kuwepo hivyo kuwa na haja ya kutafuta elimu ambayo itawanufaisha duniani na akhera.

Akifafanua kuhusu uzoefu wake katika mkutano huo wa kila mwaka, Salimatou Sabally, mjumbe wa DAUM alionyesha kufurahishwa na ujuzi alioukusanya wakati wa usomaji wa Qur'ani  ndani ya kipindi kifupi cha kuandikishwa kwake katika Jumuiya hiyo.

Fatima Sowe, Afisa Uhusiano wa Umma wa DAUM, alisema mkutano huo ni mojawapo ya mipango iliyokusudiwa kukuza urafiki na undugu miongoni mwa wanachama.

Sowe alibainisha kuwa matukio mengine ni pamoja na mashindano ya hotuba na mfululizo wa mihadhara kati ya makundi mbalimbali ya wanachama kwa maana ya kuchochea utamaduni wa kusoma na utafiti juu ya suala lolote mada.

Tukio hilo lilikuwa na mihadhara kuu ya Ustadha Mariama Sarr na Ustadha Fatima Quraysh kuhusu maingiliano ya kijamii na kukuza uhusiano.

DAUM ni shirika lisilo la kibiashara  ambalo limekuwepo kwa miaka 25 iliyopita. Inashughulikia mahitaji ya wasichana na wanawake katika kujifunza naufundishaji wa Qur’ani kwa msaada wa Taasisi ya Kiislamu ya Elimu na Maendeleo (IIED) yenye makao yake makuu Busumbula magharibi mwa Gambia.

3479132

 

captcha