IQNA

11:02 - February 04, 2021
Habari ID: 3473619
TEHRAN (IQNA) - Sera za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Ufaransa zimechukua mwelekeo mpya baada ya serikali kuanza kufunga maduka ya Waislamu kwa visingizio mbali mbali vya 'kisheria'.

Kwa mujibu  taarifa, maafisa wa serikali za mitaa Ufaransa sasa wanatumia kila kisingizio kufunga biashara za Waislamu ikiwa ni katika kutekeleza sera jumla za Rais Emmanuel Macron ambaye ameanzimia kuwadhoofisha Waislamu nchini humo.

Mwezi uliopita, kamati maalumu ya Bunge la Kitaifa la Ufaransa liliidhinisha sheria ya 'thamani za jamhuri' ambazo zilipendekezwa na rais Macron kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin amedai katika ukurasa wake wa Twitter kuwa sheria hiyo inalenga kulinda thamani za jamhuri sasa na siku za usoni.

Imedokezwa kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uaransa imezitaka idara zinazohusika na ukaguzi wa biashara kufunga migahawa na maduka ya Waislamu kusini mwa Paris kwa kutumia kila aina ya kisingizio cha 'kisheria'.

Hivi sasa Waislamu nchini Ufaransa wameingiwa na wasi wasi mmkubwa kwani baada ya serikali kuanza kufunga misikiti sasa imegukia biashara zao.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3951919

Kishikizo: ufaransa ، waislamu ، macron
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: