IQNA

Ufaransa yaidhinisha sheria ya kuwakandamiza Waislamu zaidi

11:41 - December 11, 2020
Habari ID: 3473446
TEHRAN (IQNA) -Utawala wa Ufaransa, wenye chuki shadidi dhidi ya Uislamu, umepasisha sheria mpya ya kuzidi kuwabana na kuwakandamiza Waislamu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, serikali ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, jana Alkhamisi ilipasisha sheria ya kuzidi kuwakandamiza na kuwanyanyasa Waislamu kwa madai ya kupambana na misimamo mikali na kutia nguvu thamani za Jamhuri ya Ufaransa.

Sheria hiyo ni sehemu ya hatua mbovu za Macron za kuunga mkono thamani za usekulari na kupiga vita mafundisho ya Uislamu.

Siku ya Jumatano, waziri mkuu wa Ufaransa, Jean Castex aliwasilisha muswada wa kutia nguvu thamani za Jamhuri ya Ufaransa ambazo zinapiga vita moja kwa moja mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Wakosoaji wa sheria hiyo mpya ya serikali ya Ufaransa wameonya kwamba lengo la Emmanuel Macron na serikali yake ni kuzidi kuwakandamiza Waislamu.

Wabunge wa Ufaransa wamepasisha sheria hiyo katika hali ambayo, Paris ni muungaji mkono wa magenge ya kigaidi katika maeneo tofauti duniani hasa katika nchi za Kiarabu kama vile Syria.

Tarehe 2 Oktoba mwaka huu, rais wa Ufaransa aliwasilisha mpango wa kupiga vita waziwazi Uislamu nchini humo akidai eti lengo lake ni kukabiliana na misimamo mikali. 

Sheria hiyo inapiga vita uwekezaji wowote wa kigeni unaowahusu Waislamu, kama wa kujenga misikiti na shule za Waislamu na vile vile kuwadhibiti na kuwakandamiza maimamu wa misikiti wasio na uraia wa Ufaransa.

Siasa hizo za utawala wa Ufaransa zimesababisha kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu na kuzidi kubaguliwa na kunyanyaswa Waislamu katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikijinadi kuwa eti ni kitovu cha uhuru. Hatahivyo imebainika kuwa madai hayo ni hadaa na undumakuwili.

3939979

captcha