IQNA

10:59 - April 10, 2021
News ID: 3473798
TEHRAN (IQNA)- Msikiti katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambao ulikuwa umefungwa kama sehemu ya ukandamizaji wa Waislamu baada ya kuuawa mwalimu aliionyesha katuni zilizomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, umefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda wa miezi sita.

Waumini zaidi ya 200 walikusanyika jana kwa ajili ya  Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Jamia wa Pantin wenye uwezo wa kubeba waumini 1,300.

Polisi Ufaransa walianzisha msako uliowalenga Waislamu baada ya Samuel Paty kuuawa ambapo msikiti huo mkubwa ulifungwa katika msako huo.

Siku kadhaa kabla ya kuuawa Paty msikiti huo ulio katika mtaa wa Sien-Saint-Denis ulichapisha katika ukurasa wake wa Facebook video iliyomkosoa Paty kwa kusambaza taswira zilizomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW. Mwalimu huyo aliuawa na kijana mwenye hasira mwenye asili ya Chechenia ambaye naye alipigwa risasi na kuuawa na polisi.

Hayo yanajiri wakati ambao uamuzi wa Baraza la Seneti la Ufaransa wa kupasisha mpango unaopiga marufuku wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kuvaa Hijabu katika maeneo ya umma umelaaniwa na kukosolewa vikali ndani ya nchi hiyo na katika kila pembe ya dunia.

Mswada huo umeelezwa kuwa ni sehemu ya uendelezaji wa kampeni ya kueneza chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) barani Ulaya.

Ufaransa yenye Waislamu wapatao milioni tano na laki saba, ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya.

3474403

Tags: paris ، ufaransa ، waislamu
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: