IQNA

Kiongozi Muadhamu: Nafasi ya vijana katika masuala muhimu ya nchi ni fakhari kwa Mapinduzi ya Kiislamu

17:23 - February 20, 2021
Habari ID: 3473668
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza nafasi ya kipekee ya tabaka la vijana katika masuala muhimu nchi na kueleza kuwa, uwepo wa kizazi hicho katika masuala hasasi ya nchi ni katika mafanikio na fakhari ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo katika ujumbe wake uliosomwa mapema leo na Hujjatul-Islam wal Muslimin, Ahmad Vaezi, katika kikao cha 55 cha Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Ulaya, kilichofanyika kwa njia ya intaneti.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yameacha nembo katika vifua vya vijana wa nchi hii, na hilo limedhihiri kwa namna wanavyobuni mipango na ramani ya masuala tofauti ya kimsingi ya taifa hili. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kwamba, kadiri siku zinavyopita, ndivyo umuhimu wa nafasi ya vijana katika ustawi na maendeleo ya nchi na kuwa na mustakabali wenye dhamana unvyoazidi kudhihiri.

Amesema idadi kubwa ya wanachuo waliofuzu wanafanya kazi kubwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na matunda ya hudumu zao katika maendeleo ya sayansi na teknolojia yanahisika kote nchini. Ayatullah Ali Khamenei amebainisha kuwa, janga la corona kwa mara nyingine tena, limeweka wazi ukweli huo, na kwamba ari, moyo na kujitolea vijana katika suala hilo (la kupambana na corona) kumepelekea kufunguka milango ya kupatikana ufumbuzi wa kisayansi na wa kivitendo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaasa vijana kukumbatia fursa zilizopo, wajipambe kadri wanavyoweza na ustadi katika nyuga za sayansi, dini na akhlaqi; sambamba na kujiandaa kuchukua nafasi kubwa zaidi hapo baadaye. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Ulaya una jukumu zito na tukufu katika uwanja huo.

3955107/

captcha