IQNA

16:22 - March 02, 2021
News ID: 3473696
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Saeed Mohammad Nour, maarufu kama 'Sheikh Saeed' alikuwa qarii maarufu wa Sudan ambaye kwa muda mrefu aliishi Misri na kisha akaaga dunia akiwa nchini Kuwait.

Sheikh Saeed alipata umaarufu kutokana na sauti yake nzuri na mbinu ya kipekee ya usomaji Qur'ani Tukufu.

Alisafiri Saudia na Kuwait kwa lengo la kurekodi qiraa ya Qur'ani katika radio za nchi hizo. Qarii Saeed alikuwa akisoma Qur'ani katika Msikiti wa Al-Khazandar katika eneo la Shabraa mjini Cairo.  Alikuwa na sauti yenye mvuto sana na hata watu walikuwa wakisimamisha magari yao kusikiliza sauti yake katika vipaza sauti msikitini.

 

3956952

Tags: saeed ، qurani tukufu
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: