IQNA

Israel yakosolewa kuzuia Wapalestina chanjo ya COVID-19

18:23 - April 09, 2021
Habari ID: 3473796
TEHRAN (IQNA) - Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekosoa hatua za utawala wa Israel kuzuia chanjo ya COVID-19 kufika Palestina.

Shirika la Amnesty International limesema katika ripoti yake ya kila mwaka kwamba, Israel imeendelea kukiuka sheria za kimataifa kwa kuzuia operesheni ya kupelekwa chanjo ya COVID-19 kwa Wapalestina milioni tano wanaoishi Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza. 

Hii ni licha ya kuwa, idadi ya waathirika wa COVID--19 huko Palestina inaongezeka kwa kasi kutokana na vizuizi za utawala haramu wa Israel na uhasama wake dhidi ya Wapalestina. Hadi sasa Wazayuni wa Israel wanaendelea kuzuia hatua yoyote ya kupelekwa chanjo ya corona kwa raia wa Palestina. Viongozi wa utawala haramu wa Israel wametangaza kuwa, hawataruhusu kuingizwa chanjo hiyo katika eneo la Ukanda wa Ghaza.

Wakati huo huo makundi ya mapambano ya ukombozi wa Palestina yameitahadharisha Israel kutokana na hatua yake ya kuzuia chanjo ya corona kwa Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. 

Taarifa iliyotolewa na makundi hayo imesisitiza kuwa, walimwengu hususan Shirika la Afya Duniani (WHO) wanapaswa kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel na kuulazimisha uruhusu kupeleka chanjo ya COVID-19 kwa Wapalestina Ukanda wa Ghaza.  

3963282

captcha