IQNA

Muqtada Sadr ataka kuwepo mazungumzo baina ya Iran na Saudia

14:14 - June 22, 2021
Habari ID: 3474031
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi mwandamizi wa Kiislamu nchini Iraq Sayyid Muqtada al Sadr ametoa wito kwa Iran na Saudi Arabia kutatua hitilafu zao kupitia mazungumzo.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter, al Sadr amesema nchi hizi ni majirani na ni madola yenye nguvu na uwezo katika eneo n azote zina ushirikiano mzuri na Iraq.

Ameongeza kuwa, Iraq inaweza kuwa mpatanishi baina ya Saudia na Iraq.

 Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raeisi jana akizungumza na waandishi habari alisema  Iran inataka uhusiano mzuri na nchi zote za jirani, haswa Saudi Arabia. Alisema uhusiano mwema na nchi jirani ni jambo ambalo linapewa kipaumbele na Iran na hivyo hakuna kizingiti chochote katika kuanzisha tena uhusiano na Saudia.

3979204

Kishikizo: iran raeisi
captcha