IQNA

Bi kizee wa miaka 90 aliyehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu Misri

14:06 - June 26, 2021
Habari ID: 3474043
TEHRAN (IQNA)- Bi kizee aliye na umri wa miaka 90 nchini Misri amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na ana uwezo wa kusoma kwa mbinu 10 tafauti.

Bi. Ruhiya Arafah Manosur ana ujuzi wa hali ya juu katika uga wa Qur'ani Tukufu na ni miongoni mwa wanaotoa idhini au ijaza kwa wanaotaka kuanza shughuli ya  kuwa qarii.

Alizaliwa mwaka 1931 katika mkoa wa Dakahlia kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Misri, Cairo. Baba yake alikuwa afisa wa polisi na alimpeleka kwa chuo cha hafidh wa Qur'ani mtajika wakati huo Sheikh Abdulghani Goma akiwa na umri wa miaka 7 ili apate mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani.

Aliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu baada ya miaka miwili na aliendelea kwa miaka mingine mitano ambapo alijifunza mbinu 10 za qiraa. Mwanamke huyu mwenye ulemavu wa macho amekuwa akiisi katika kijiji alikozaliwa huku akitoa mafunzo ya Qur'ani kwa watoto na wengine.

Sheikha Ruhiya ambaye mwaka huu ametimia umri wa miaka 90 angali amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na anaendele akutoa mafunzo kwa vizazi vijavyo.

بانوی 90 ساله نابینای مصری؛ حافظ قرآن با قرائات دهگانه + عکس
 
بانوی 90 ساله نابینای مصری؛ حافظ قرآن با قرائات دهگانه + عکس
 
بانوی 90 ساله نابینای مصری؛ حافظ قرآن با قرائات دهگانه + عکس
 
بانوی 90 ساله نابینای مصری؛ حافظ قرآن با قرائات دهگانه + عکس 

3979569

Kishikizo: misri qarii
captcha