IQNA

Makala 21 zawasilishwa katika Kongamano la Muujiza wa Kisayansi wa Qur’ani na Sunnah nchini Misri

20:38 - October 25, 2024
Habari ID: 3479642
IQNA - Kongamano la kimataifa la Muujiza wa Kisayansi Ndani ya Qur'an na Sunna za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) limepangwa kufanyika nchini Misri baadaye mwezi huu.

Kongamano hilo litafanyika Oktoba 26-27, na limeaandaliwa na Jumuiya ya Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar.
Wasomi na watafiti kutoka Misri na nchi nyingine 9 za Kiarabu na Kiislamu wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
Kutakuwa na vikao 6 vya kielimu kuhusu vipengele tofauti vya muujiza wa kisayansi katika Quran na Sunnah za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).
Kwa mujibu wa Ali Fuad Mukhaymir, rais wa mkutano huo, makala zitakazowasilishwa zinazingatia ushahidi wa kisayansi kuhusu miujiza ya Qur’ani na Sunnah.
Ufafanuzi, kanuni na matokeo ya muujiza wa kisayansi, uumbaji wa mwanadamu kutoka kwa udongo, Makka kuwa kitovu cha dunia, na muujiza wa balagha ya Qur’ani ni miongoni mwa mada za makala, alisema.
Qur’ani Tukufu ina miujiza mingi ya kisayansi ambayo imewashangaza wanasayansi katika nyanja mbalimbali.
Muujiza wa kisayansi ni miongoni mwa vipengele vikuu vya miujiza ya Qur’ani katika zama za leo. Aya nyingi za Qur’ani zinataja masuala ya kisayansi. Kwa vile baadhi ya maswala haya yalikuwa hayajagunduliwa wakati wa kuteremshwa kwa Qur’ani na watu kupatikana kuyahusu karne nyingi tu baadaye, yanazingatiwa kama sehemu ya muujiza wa Qur’ani Tukufu.
Qur’rani kitabu ambacho siri zake zinazidi kubainika kadiri muda unavyosonga mbele.

3490404

Habari zinazohusiana
captcha