IQNA

Harakati ya Qur'ani

Idhaa ya Qur'ani ya Misri ni maarufu zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu

17:59 - August 10, 2024
Habari ID: 3479259
IQNA - Mkurugenzi wa zamani wa Redio ya Qur'ani ya Misri ameieleza idhaa hiyo kuwa maarufu zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.

Ridha Abdul Salam alisema licha ya ushindani mkubwa, Redio ya Qur'ani ya Misri bado ina idadi kubwa zaidi ya wasikilizaji kati ya vituo vya redio vya Kiarabu, Akhbar al-Yawm iliripoti.

Alisema aliwahi kuwa mkuu wa Redio ya Qur'ani Tukufu kwa muda wa miaka mitatu na kuongeza kuwa ni heshima kwake kuhudumu katika nafasi hiyo.

"Nilifanya juhudi nyingi kudumisha nafasi inayoongoza ya redio," aliongeza.

Abdul Salam pia alisisitiza haja ya kutumia teknolojia ya hali ya juu katika utayarishaji na utangazaji wa vipindi vya redio.

Katika maelezo yake ameashiria utangazaji wa usomaji adimu wa Qur'ani Tukufu unaofanywa na redio hiyo na kusema mfululizo wa visomo hivyo vya qari nguli Abdul Basit Abdul Samad vimetolewa kwa ajili ya Redio ya Qur'ani na familia ya qari.

Alisema kamati inapitia na kutathmini visomo ili viwe tayari kwa matangazo.

Kuna mfululizo mwingine uliokaririwa na qari mwingine mashuhuri Sheikh Mahmoud Khalil Al-Hussary ambao pia unakaguliwa ili kutangazwa, aliendelea kusema.

Redio ya Qur'ani ya Misri ilianzishwa mnamo 1934 kwa madhumuni ya kuzuia upotoshaji wa Qur'ani Tukufu na kutoa usomaji sahihi wa Kurani kwa qaris mashuhuri.

Tangu kuanzishwa kwake, idhaa hiyo ya Qur'ani imekuwa maarufu sana kwa watu wa Misri na pia nchi zingine ulimwenguni.

4230868

Habari zinazohusiana
Kishikizo: idhaa ya qurani misri
captcha