IQNA

Wizara ya Awqaf Misri, Akademia ya Fiqhi kushirikiana kukabiliana na ‘misimamo mikali’

13:03 - July 07, 2021
Habari ID: 3474077
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Awqaf nchini Misri Sheikh Mukhtar Gomaa amekutana na Katibu Mkuu wa Akademia ya Kimataifa ya Fiqhi Sheikh Koutoub Mustafa Sano kujadili njia ya kukabiliana na misimamo mikali ya kidini.

Katika kikao ambacho kimefanyika katika makao makuu ya academia hiyo mjini Jeddah, Saudi Arabia, wawili hao wamesisitiza kuhusu ulazima wa kushirikiana kukabiliana na ‘idiolojia zenye misimamo mikali’.

Aidha wamebadilihsana mawazo kuhusu kustawisha mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW na halikadhalika kukuza utamaduni wa Kiislamu duniani.

Waziri Gomaa amemtunuku Sheikh Sano vitabu kadhaa ambavyo vimechapishwa na Wizara ya Awqaf na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Misri.

Akademia ya Kimataifa ya Fiqhi ni taasisi ya kimataifa ya Kiislamu ambayo ilianzishw akwa ajili ya kufanya utafiti wa ngazi za juu kuhusu fiqhi ya Kiislamu na sheria na inadesha shughuli zake chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

همکاری اوقاف مصر و مجمع فقه اسلامی جده برای مقابله با اندیشه‌های افراطی
 
همکاری اوقاف مصر و مجمع فقه اسلامی جده برای مقابله با اندیشه‌های افراطی

 

3475166

captcha