Mufti Abubakar bin Zubeir amesema hayo katika mazungumzo yake na Dr. Mohsen Maarefi, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania ambapo amewashukuru wasimamizi wa Qur'an wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika kikao hicho, Mufti wa Tanzania alialikwa kufungua rasmi akademia hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO), Mufti Zubeir amesema kuwa, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) halitaacha kamwe kusaidia juhudi zozote (zinazohitajika) katika mwelekeo huu, na akasisitiza kuwa atashiriki kwa fahari kubwa katika hafla ya ufunguzi.
Kadhalika Sheikh Mkuu wa Tanzania amesema kuwa, mpango huu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuzingatia zaidi programu za Qur'ani utapelekea kukuza elimu na utamaduni wa Qur'ani kwa watu wa Tanzania.
Katika Akademia ya Qur'ani ya Dar al-Nur kutaendeshwa kozi mbalimbali kama za: Uandishi wa Qur'an nchini Tanzania, maonyesho makubwa ya Qur'an jijini Dar-es-Salaam, mafunzo ya mbinu ya Kuhukumu Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an katika Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania, na kusaidia katika kutuma wasomaji wateule wa Iran kwenda kushiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an nchini Tanzania, Mbinu ya Kuhifadhi Qur'an hasa kwa Wanawake wa Dar-es-Salaam, na kuwapeleka Iran Wasomaji watano bora wa Kitanzania kwa ajili ya mafunzo ya juu zaidi ya sauti na lahani ya usomaji Qur'ani.
Hivi karibuni Hujjatul Islam Hosseini Neyshabouri, Mkuu wa Kituo cha Kituo cha Kimataifa cha Qu'rani na Uenezi cha ICRO amesema Akademia ya Qur'ani ya Dar An-Nur itatoa mafunzo kwa wanafunzi hapo Dar na kusaidia kuimarisha vituo vya mafunzo ya Qur'ani vya mkoa huo.
Amesema akademia hiyo itaandaakozi na programu mbalimbali za ana kwa ana na za mtandaoni katika nyanja kama vile qiraa, kuhifadhi, kutafakari maana ya aya za Qur'ani n.k.
Aidha amesema Qur’ani Tukufu imeteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu kwenye wokovu na ukamilifu.
3490929