IQNA

Kongamano la Misri lajadili suala la utoaji wa fatuwa

20:03 - October 18, 2018
Habari ID: 3471711
TEHRAN (IQNA)-Kongamano moja la kimataifa limefanyika Cairo, Misri kwa lengo la kujadili kadhia ya utoaji wa fatuwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kongamano hilo la siku mbili ambalo lilifanyika chini ya anuani ya 'Bidaa katika Utoaji wa Fatuwa", lilifunguliwa Jumanne na Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri. Kongamano hilo limehudhuriwa na wanazuoni, mamufti na viongozi wa kidini kutokana nchi zaidi ya 73.
Kati ya waliohutubu katika kongamano hilo ni Mufti wa Misri Sheikh Shawki Allam na Waziri wa Wakfu wa Misri Sheikh Mokhtar Gomaa.

3756405

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha