IQNA

Vita vya Saudia vinaua mtoto kila dakika 10 nchini Yemen

18:27 - August 24, 2021
Habari ID: 3474223
TEHRAN (IQNA)- Hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya nchini Yemen kutokana na vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu na kusema kuwa, mtoto mmoja wa Yemen hupoteza maisha kila baada ya dakika 10.

Katika hotuba yake, ameongeza , "Nchini Yemen, mtoto mmoja anafariki dunia ndani ya kila dakika 10 kutokana na sababu zinazozuilika kama vile utapiamlo na magonjwa yanayoweza kudhibitiwa kupitia chanjo."

Amebainisha kuwa, "Miaka 6 iliyopita, watu wazima walianzisha vita Yemen. Walichukua hatua hiyo licha ya kufahamu matokeo mabaya ya migogoro ya namna hii kwa watoto wadogo."

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa UNICEF amekumbusha kuwa, watoto milioni 11.3 wa Yemen wanahitajia misaada ya kibinadamu, huku milioni 2.3 miongoni mwao wakisumbuliwa na utapiamlo wa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lishe duni miongoni mwa watoto wa Yemen walio chini ya umri wa miaka mitano ni ya kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia.

Aidha hivi karibuni Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ulionya kuwa, mustakabli wa elimu ya watoto zaidi ya milioni 6 nchini Yemen upo hatarini kwani watoto hao wamo katika hatari ya kukosa masomo kutokana na kushindwa kwenda shuleni.

Mwezi Juni mwaka huu,  Watoto wa Yemen waliandamana mjini Sanaa kulaani vikali uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa muungano vamizi wa Saudia baada ya umoja huo kukataa kukosoa Saudia na waitifaki wake wanaotenda jinai dhidi ya watoto Wayemeni.

Utawala dhalimu wa Saudia ulianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mnamo Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Makumi ya maelefu ya watu wa Yemen, hasa wanawake na watoto wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita hivyo huku Malaki au hata mamilioni yaw engine wakipoteza maisha kutokana na maafa na majanga yaliyosababishwa na vita hivyo. Watoto Wayemen ndio waathirika wakuu kwani wengi wamekosa lishe, dawa na matibabu kutokana na vita hivyo vya Saudia dhidi ya nchi yao.

3475565

Kishikizo: yemen saudia watoto
captcha