IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Nepal yafikia fainali mjini Katmandu

14:37 - November 17, 2025
Habari ID: 3481530
IQNA-Duru ya tatu kwa mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani nchini Nepal imeingia hatua ya mwisho, Jumapili. Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da‘wa na Mwongozo ya Saudi Arabia imezindua raundi ya mwisho ya mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kwa wavulana na wasichana katika mji mkuu wa Katmandu, ulioko Asia Kusini.

Awamu ya awali ya mashindano haya ilishuhudia ushiriki mpana, zaidi ya washiriki 800, ambapo 189 walistahiki kuingia fainali ya siku tatu. Mashindano haya ni sehemu ya juhudi za wizara kueneza maadili ya Qur’ani Tukufu miongoni mwa vijana na kuunga mkono programu za hifdh na qira’a ndani ya jamii za Kiislamu.

Nepal ni nchi isiyo na pwani, iliyoko katikati ya milima ya Himalaya katika Asia Kusini. Uislamu ni dini ya wachache nchini humo. Kwa mujibu wa sensa ya Nepal ya mwaka 2011, Waislamu ni asilimia 4.4 ya idadi ya watu. Takribani asilimia 97 ya Waislamu wanaishi katika eneo la Terai, huku asilimia 3 iliyosalia ikipatikana zaidi mjini Katmandu na katika milima ya magharibi.”

3495420

Kishikizo: nepal qurani tukufu
captcha